Benki ya NMB jana ilianza maadhimisho ya miaka 10 tangu kubinafsishwa huku ikiweka bayana mafanikio makubwa iliyoyapata ikiwemo kuongeza matawi kutoka chini ya 100 miaka 10 iliyopita mpaka matawi 173 leo hii, kutoka kutokuwa na ATM mpaka ATM zaidi ya 600 na wateja kufikia zaidi ya milioni 2 kutoka laki 6 miaka 10 iliyopita. NMB pia imefanikiwa kuwa na matawi katika kila wilaya nchini.

Mkurungenzi wa NMB – Ineke Bussemaker akiwa na Raisi Jakaya Kikwete katika matukio mawili tofauti. Tukio la kwanza lilikuwa jijini Arusha kwenye mkutano mkuu wa wadau wa barabara ambapo NMB ilikuwa mdhamini mkuu, mkutano huo uliwakutanisha viongozi wa mikoa na halmashauri zote nchini ambapo Mh Raisi Kikwete alikuwa mgeni rasmi.

Mkurugenzi  Mtendaji  wa NMB-Ineke Bussemaker akitangaza matokeo ya kifedha ya nusu mwaka mbele ya Waandishi wa Habari katika Ofisi Mpya za NMB Makao Makuu jana. NMB ilitanganza faida baada ya kodi ya shilingi bilioni 77 ikiwa zaidi ya faida ya mwaka jana kipindi hicho hicho ambayo ilikua shilingi bilioni 72/-. Kushoto ni Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB-Waziri Barnabas.

  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.Felix Tibenda (pili kushoto) akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa NMB Bi. Ineke Bussemaker kwa uzinduzi wa NMB Mastercard kwa Mkoa wa Arusha na Kanda nzima ya Kaskazini. Wakishuhudia ni Meneja wa NMB kanda ya Kaskazini Bw.Salie Mlay(kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi Bw.Abdulmajid Nsekela .

Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya kikwete akimkabidhi Mtendaji Mkuu wa NMB Bi Ineke Bussemaker kikombe cha mahindi wapili kundi la taasisi za kibenki zilizoshiriki maonesho ya Nane nane Kitaifa 2015 katika viwanja vya Ngongo Lindi.