(NMB), Benki inayoongoza kwa kuwa na wateja wengi nchini, imezindua rasmi familia ya kadi za benki “MasterCard Debit”, zikiwemo Tanzanite, Titanium  kwa mara ya kwanza nchini Tanzania, Kadi ya “First world Rewards”.  

 

Familia hii ya kadi hizi za benki zitahudumia wateja aina mbalimbali, ikiwemo asilimia kubwa ya wateja (Tanzanite), wateja wa kipato cha kati (Titanium) na wale wateja wa kipato cha juu (World Rewards) ikitoa huduma na faida mbalimbali mahususi kwa walengwa.

“Pamoja na ukuaji wa kasi katika sekta ya malipo kwa njia ya elektroniki, wateja wetu wanazaidi kutafuta njia za haraka, salama na zenye unafuu kutumia katika malipo. Kukabiliana na wimbi hili, tumezindua familia hii ya kadi zinazokubalika kimataifa, na hivyo kurahisisha upatikanaji wa pesa zao kwa usalama popote walipo, Tanzania au nje ya nchi” alisema Ineke Bussemaker, Mkurugenzi mtendaji wa NMB.

Wamiliki wa kadi hizi za ‘MasterCard’ wataweza kutoa Fedha kutoka mashine za Miamala ya fedha duniani kote zenye alama ya “MasterCard Acceptance” ya fedha. Pia wataweza kulipia bili, kulipia umeme na Salio za simu, pamoja na kununua bidhaa mtandaoni kutoka maduka mbalimbali makubwa ndani na je ya nchi.

“Kadi za “MasterCard debit” zinakubalika na mamilioni ya wafanya biashara kutoka nchi Zaidi ya 210, ikiwa na maana kuwa wanaosafiri kwa ajili ya mapumziko au biashara wataweza kupata pesa zao popote pale, kwa urahisi kama wakiwa nyumbani” alisema Michael Miebach, Raisi, Mashariki ya kati na Africa, MasterCard. “muhimu Zaidi, kila muamala wa kitaifa na kimataifa unalindwa na usalama wa “masterCard SecureCode pamoja na EMV chip na Teknolojia ya PIN” ambazo hutoa usalama wa ziadakila mara mteja anatumia kadi yake mtandaoni au katika duka la kawaidia.”

NMB pia inakuwa Benki ya kwanza Tanzania kuzindua kadi ya “MasterCard World Rewards”. Kadi hii inawapa fursa wamiliki kupata huduma za kipekee za kiamisha kama vilie ofa za ndege, malazi, kukodisha gari, vyakula, manunuzi, michezo na burudani kupitia “Mastercard priceless Cities and Priceless Africa Programmes”.

“Hapa NMB tunaamini ni muhimu kufahamu mahitaji na matakwa ya wateja wetu, na kuwazawadia kutokana uaminifu wao. Tunayofuraha kuwa benki ya kwanza Tanzania kutambulisha mpango huu wakimapinduzi unaotoa zawadi kwa wateja wetu wa kipato cha juu huduma mbalimbali za kipekee za kimaisha, kupitia matawi yetu yaliyopo tayari na tawi letu jipya kabisa la “Private banking” litakalo hudumia wateja wetu wa kipato cha juu” alisema Bussemaker.

Wamiliki wa kadi za “Worlds Rewards” wataweza kujipatia poinyti za uaminifu kila mara wanapotumia kadi zao. Pointi hizi za uaminifu zinaweza kukombolewa kwenye mashirika ya ndege zaidi ya 800 dunia nzima, kampuni za kukodisha magari an hoteli maarufu Zaidi ya 160,000 duniani.  

Wamiliki wa kadi zilizo kwenye familia hii, wataenedlea kufurahia huduma nyinginezo za NMB zikiwemo “NMB App, NMB Internet Banking, NMB E-Statement na NMB Mobile”.

-MWISHO-

Kuhusu NMB

National Microfinance Bank (NMB) ndio benki ya biashara  inayoongoza kwa huduma zote kamilifu hapa Tanzania ikitoa huduma mbalimbali za kibenki kwa kundi la wateja linalowakilisha vyema Tanzania nzima. Benki hii hutoa huduma kama za akiba, mialama pamoja na huduma za ufadili kwa watu binafsi, kuanzi kampuni ndogo hadi za kati, serikali, kilimo biashara pamoja na makampuni makubwa na taasisi. NMB pia ina jukumu muhimu katika sekta ya kilimo pamoja na maghala hapa nchini kupitia SACCOS na Amcos.

 

Katiaka Ubinafsishaji mwaka 2005, benki ilikuwa na wateja takribani 600,000, idadi hiyo ikiongezeka na kufikia millioni 1.8. Benki haikuwa na Mashine ya muamala (ATM) hata moja miaka mitano iliyopita, leo hii inamiamala Zaidi ya 600, ambayo ni asilimia 40 ya mashine zote Tanzania kwa ujumla. Benki inamatawi zaidi ya 170 na inapatikana katika asilimia 95 ya wilaya zote za kiserikali Tanzania. Nia ya benki hii ni kufikia asilimia 100 ya wilaya zote Tanzania

 

Fuatilia ukurasa wetu Twitter @NMBTanzania na upande wa Facebook NMB Tanzania