Benki ya NMB imetoa msaada wa vifaa vya hospitali kwaajili ya zahanati ya chuo kikuu cha Dodoma vyenye thamani ya Shilingi milioni 20.    Vifaa hivyo vilivyotolewa kwa Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Dodoma – Prof Shaaban Mlacha ni pamoja na - Jokofu kwaajili ya benki ya Damu, Meza ya upasuaji (Operating Table), Taa maalumu za kwenye chumba cha upasuaji (Overhead Operating Lamp) vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 20.    Msaada huo ulipokelewa vyema na uongozi wa chuo kikuu cha Dodoma kusifu juhudi za benki ya NMB katika kuchangia maendeleo nchini.  

Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa NMB, Bw. Abdulmajid Nsekela (kushoto), akimuonyesha mfano na kumpa maelezo ya kadi mpya ya NMB MasterCard Katibu Mkuu Kiongozi- Balozi Ombeni Sefue.

(NMB), Benki inayoongoza kwa kuwa na wateja wengi nchini, imezindua rasmi familia ya kadi za benki “MasterCard Debit”, zikiwemo Tanzanite, Titanium  kwa mara ya kwanza nchini Tanzania, Kadi ya “First world Rewards”.  

Benki ya NMB imekabidhi gawio la shilingi Bilioni 16.5 kwa serikali kupitia wizara ya fedha. Gawio hilo lilipokelewa na Waziri wa fedha – Saada Mkuya mbele ya katibu mkuu wa wizara ya fedha - Dr Servacius Likwelile na Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB – Waziri Barnabas. 

Serving our customers is our pride; yesterday 19th March 2014 we officially launched NMB Sinza aiming to get over 300 customers residing at Sinza location to access financial services close to their doorsteps