Mkurungenzi wa NMB – Ineke Bussemaker akiwa na Raisi Jakaya Kikwete katika matukio mawili tofauti. Tukio la kwanza lilikuwa jijini Arusha kwenye mkutano mkuu wa wadau wa barabara ambapo NMB ilikuwa mdhamini mkuu, mkutano huo uliwakutanisha viongozi wa mikoa na halmashauri zote nchini ambapo Mh Raisi Kikwete alikuwa mgeni rasmi.

 

Tukio la pili ni uongozi wa NMB ulipomtembelea rais kikwete Ikulu ya Dar es Salaam kwaajili ya utambulisho na pia kumuonesha Mh Rais huduma mbalimbali zinazopatikana kwenye kadi mpya za NMB MasterCard.

 

 

 

 

 

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania – Dr Jakaya Kikwete akipata maelezo jinsi NMB MasterCard inavyofanya kazi na faida za kutumia kadi hiyo ndani na je ya Tanzania kutoka kwa Mkurugenzi wa NMB – Ineke Bussemarker ikulu ya Dar es Salaam. Mkurugenzi huyo wa NMB alimtembelea raisi Kikwete Ikulu kwaajili ya kujitambulisha na pia kumueleza kuhusu kadi mpya za benki hiyo zilizozinduliwa hivi karibuni za NMB MasterCard.

 

 

 

 

 

 

Raisi Jakaya Kikwete akisalimiana na mkurugenzi wa NMB – Ineke Bussemaker muda mfupi kabla ya Raisi kikwete hajafungua mkutano mkuu wa mwaka wa wadau wa barabara jijini Arusha wiki iliyopita.