Raisi Jakaya Mrisho Kikwete amezindua rasmi jengo jipya na la kisasa kabisa ambalo ni makao makuu mapya ya NMB lenye ghorofa saba huku likiwa na uwezo wa kubeba wafanyakazi zaidi ya 800. Mbali na uzinduzi wa jengo hilo, Raisi Kikwete pia alizindua tawi jipya la benki lililo ndani ya jengo jipya la NMB.  

Benki ya NMB imeidhamini timu ya Taifa ya mchezo wa Hockey katika mashindano ya Africa Olympic Qualifier yatakayofanyika kuanzia Oktoba 23, 2015 mpaka Novemba 1, 2015 – Johannesburg, Afrika Kusin iikiwa na lengo la kuinua maisha ya wanawake kupitia michezo.