Mkurugenzi Mtendaji wa NMB-Ineke Bussemaker akitangaza matokeo ya kifedha ya nusu mwaka mbele ya Waandishi wa Habari katika Ofisi Mpya za NMB Makao Makuu jana. NMB ilitanganza faida baada ya kodi ya shilingi bilioni 77 ikiwa zaidi ya faida ya mwaka jana kipindi hicho hicho ambayo ilikua shilingi bilioni 72/-. Kushoto ni Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB-Waziri Barnabas.