Raisi Jakaya Mrisho Kikwete amezindua rasmi jengo jipya na la kisasa kabisa ambalo ni makao makuu mapya ya NMB lenye ghorofa saba huku likiwa na uwezo wa kubeba wafanyakazi zaidi ya 800. Mbali na uzinduzi wa jengo hilo, Raisi Kikwete pia alizindua tawi jipya la benki lililo ndani ya jengo jipya la NMB.

 

 

Uzinduzi wa jengo la makao makuu ya NMB ni mwendelezo wa maadhimisho ya Miaka 10 ya NMB ambayo yameadhimishwa kwa mafanikio makubwa. Baadhi ya mafanikio ya benki hiyo ni pamoja na kukuza mtaji wake mpaka kuwa benki kubwa na bora kuliko zote nchini huku ikiwekeza vya kutosha katika tekinolijia ya mawasiliano inayowezesha benki kumudu kutoa huduma bora na karibu zaidi ya wateja wake.

 

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania – Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa jengo jipya la makao makuu ya NMB na tawi jipya la NMB Private Banking kwenye jengo la makao makuu ya NMB jana jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia tukio hilo ni Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa NMB – Prof. Joseph Semboja(kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa NMB – Ineke Bussemaker (wapili kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam – Saidi Meck Sadiki (kulia) pamoja na wafanyakazi wa NMB.

 

 

 

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania – Dr. Jakaya Kikwete katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa NMB – Idara ya huduma kwa wateja. Raisi Kikwete alikuwa anakagua Jengo jipya la NMB ambao ndimo makao makuu mapya ya benki hiyo kubwa kuliko zote nchini.