Benki ya NMB imeidhamini timu ya Taifa ya mchezo wa Hockey katika mashindano ya Africa Olympic Qualifier yatakayofanyika kuanzia Oktoba 23, 2015 mpaka Novemba 1, 2015 – Johannesburg, Afrika Kusin iikiwa na lengo la kuinua maisha ya wanawake kupitia michezo.

 

Udhamini huo ni pamoja na kutoa tiketi za ndege kwa wachezaji wote na viongozi pamoja na vifaa vya michezo ikiwemo jezi na mavazi ya safari kwenda Afrika ya Kusini vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 17.

Afisa wa Fedha wa NMB – Waziri Barnabas alisema benki ya NMB mara zote hufarijika inapopata nafasi ya kusaidia michezo kwani kwakufanya hivyo inaonyesha kujali kwao kwani miongoni mwa wapenda michezo na wachezaji wenyewe, ni wateja wa NMB.

 

 

 

Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB – Waziri Barnabas (wapili kulia) akimkabidhi jezi Kapteni waTimu yaTaifa ya Hockey-Wanawake – Kidawa Abdallah (watatukushoto) leo katika mkutano na waandishi wa habari ambapo NMB ilitangaza udhamini wake kwaTimu yaTaifa ya Hockey inayotarajiwa kushiriki mashindano ya Afrika kuwania kufuzu mashindano ya Olimpiki (Olympic Qualifier) mashindano yatakayoanza Oktoba 23 mwaka huu. Wakishuhudia kutoka kushoto nI Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Michezo – Juliana Soda na Kocha wa Timu ya Taifa ya Hockey – Wanawake – Valentina Quaranta (kulia).

 

 

 

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Michezo – Juliana Yasoda (Wapili kushoto) akikabidhi bendera ya taifa kwa Kapteni wa Timu yaTaifa ya Hockey