Benki ya NMB imekabidhi gawio la shilingi Bilioni 16.5 kwa serikali kupitia wizara ya fedha. Gawio hilo lilipokelewa na Waziri wa fedha – Saada Mkuya mbele ya katibu mkuu wa wizara ya fedha - Dr Servacius Likwelile na Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB – Waziri Barnabas. 

 

Benki kupitia mkutano mkuu wa mwaka iliidhinisha shilingi Bilioni 52 kama gawio kwa wanahisa wake ikiwa ni sehemu ya faida iliyopatikana kwa mwaka 2014.

Gawio hilo ni kutokana na faida ya shilingi Bilioni 156 baada ya kodi iliyopatikana kwa mwaka 2014. Faida hiyo na gawio lililoidhinishwa ni Faraja kwa wanahisa wanaojivunia benki bora yenya matawi mengi kuliko benki yoyote Tanzania ikiwa na matawi zaidi ya matawi 163 na ATM zaidi ya 550 huku huduma zake zikiwa zimeenea kila wilaya hapa nchini.

Mkurugenzi Mkuu wa NMB – Ineke Bussemaker akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi Bilioni 16.5 kwa Waziri wa Fedha – Saada Mkuya katika hafla iliyofanyika juzi mjini Dodoma. NMB ilikabidhi fedha hizo kwa serikali ikiwa ni gawio la sehemu ya faida iliyopatikana kwa mwaka 2014 ya shilingi Bilioni 155.6 huku bodi ya wakurugenzi ikipitisha gawio la wanahisa la shilingi bilioni 52. Kutoka kushoto ni katibu mkuu wa wizara ya fedha - Dr Servacius Likwelile na kulia ni Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB – Waziri Barnabas.