Benki ya NMB imetoa msaada wa madawati 100 yenye thamani ya shilingi milioni 10 kwa shule mbili za msingi mkoani Dodoma kwaajili ya kukabiliana na adha ya ukosefu mkubwa wa madawati kwenye shule hizo.

 

Msaada huo ulikabidhiwa kwa walimu wakuu wa shule za msingi Chikowa na Mwenge ikiwa ni mwendelezo wa Benki katika kuchangia huduma za kijamii kwa njia ya kurudisha sehemu ya faida inayopatikana.

Afisa Elimu shule za msingi katika Manispaa ya Dodoma – Scola Kapinga aliimwagia sifa NMB na kuitaja kuwa ni benki inayoongoza kuchangia huduma za jamii kuanzia elimu, afya na hata kusaidia wananchi wanapopata majanga kama mafuriko.

“Serikali inatambua na kuuthamini sana mchango wa NMB katika kuchangia huduma za jamii kama ilivyo leo hii ambapo mmetusaidia madawati 100 kwaajili ya shule za msingi hizi za mwenge na chikowa zenye upungufu mkubwa wa madawati.” Alisema Bi Scola na kuongezea kuwa Madawati hayo yatasaidia katika kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia.

Akikabidhi madawati hayo, Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya NMB – Waziri Barnabas alisema kuwa NMB iliguswa na upungufu mkubwa wa madawati katika shule hizo na kuamua kuwasaidia ili kupunguza makali ya upungufu wa madawati huku akiweka bayana kuwa kwa mwaka 2016, NMB imetenga zaidi ya shilingi bilioni moja na nusu (Bilioni 1.5) kwaajili ya kuchangia huduma za elimu, afya na kukabiliana na majanga kama mafuriko.

Kwa mwaka huu tayari NMB imenunua madawati 300 kwa mikoa ya Singida, Dodoma na Manyara huku ikitoa vifaa vya hospitali kwa hospitali ya Mkoa wa Singida, tunategemea pia kutoa mashuka 150 kwa hospitali ya Mkoa wa Dodoma hivi karibuni”alisema Waziri.

 

Afisa mkuu Fedha wa NMB – Wazir Barnabas (Kulia) akimkabidhi madawati mwalimu mkuu wa Shule ya msingi Mwenge – Baraka Gongo huku Afisa Elimu shule za msingi wa Manisapaa ya Dodoma – bi Scola Kapinga akishuhudia katika hafla ya kukabidhi madawati iliyofanyika shuleni hapo siku ya jumamosi. NMB ilikabidhi madawati 100 yenye thamani ya shilingi Milioni 10 kwa shule za msingi Mwenge na Chikowa zilizopo manispaa ya Dodoma ikiwa ni mpango wa benki katika kusaidia maendeleo ya jamii kwa kuhakikisha wanatenga  sehemu ya faida wanayoipata kusaidia maendeleo ya jamii.

 

 

 

Afisa mkuu Fedha wa NMB – Wazir Barnabas (Kulia) akimkabidhi madawati mwalimu mkuu wa Shule ya msingi Chikowa – Andrew Seth huku Meneja wa  NMB kanda ya Kati – Straton Chilongola akishuhudia katika hafla ya kukabidhi madawati iliyofanyika katika shule ya msingi Mwenge ya jumamosi. NMB ilikabidhi madawati 100 yenye thamani ya shilingi Milioni 10 kwa shule za msingi Mwenge na Chikowa zilizopo manispaa ya Dodoma ikiwa ni mpango wa benki katika kusaidia maendeleo ya jamii kwa kuhakikisha wanatenga  sehemu ya faida wanayoipata kusaidia maendeleo ya jamii.

 

 

 

Wanafinzi wa shule za msingi Mwenge na Chikowa wakiwa wamekaa kwa furaha kwenye madawati yaliyotolewa na benki ya NMB muda mchache baada ya madawati hayo kuwasili shuleni kwao. NMB ilikabidhi madawati 100 yenye thamani ya shilingi Milioni 10 kwa shule za msingi Mwenge na Chikowa zilizopo manispaa ya Dodoma ikiwa ni mpango wa benki katika kusaidia maendeleo ya jamii kwa kuhakikisha wanatenga  sehemu ya faida wanayoipata kusaidia maendeleo ya jamii.

 

 

 

Mwenge Primary school students in Dodoma carrying Desks moments after NMB had donated school desks to Mwenge and Chikowa Primary schools as a way of the bank’s initiative of addressing school desks challenge in primary and secondary schools in the country. NMB Donated 100 desks worth TZS 10 Million to Mwenge and Chikowa primary schools in the quest to help address the school desks shortage in the schools.