NMB imetoa msaada wa vifaa vya hospitali kwa hospitali ya wilaya ya Magu iliyopo mkoani Mwanza  ikiwa ni harakati za kuhakikisha kuwa benki inawafikia wananchi wengi Zaidi na mahali popote walipo bila kujali umbali.

Msaada huo uliotolewa ni vitanda vya kawaida na kujifungulia wakina mama wajawazito vyenye thamani ya shilingi Milioni 5. NMB inatambua kuwa ni kupitia jamii ndipo wateja wao mwengi wanapotoka, kwa hiyo kurudisha sehemu ya faida kwa jamii ni sehemu ya utamaduni wao.

 

Mkurugenzi Mtendaji wa NMB – Ineke Bussemaker akikabidhi vitanda vya hospitali kwaajili ya hospitali ya wilaya ya Magu kwa mkuu wa wilaya hiyo – Bi Karen Kemilembe. Mwishoni mwa wiki, NMB ilitoa vitanda vya kawaida na vya kujifungulia kwa hospitali hiyo ili kukabiliana na uhaba wa vitanda kwa wagonjwa na wadi ya akina mama wajawazito. Wanaoshuhudia ni Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa – Abraham Augustino (mwenye tai) na Mkurugenzi wa wilaya ya Magu - William Ntinika

 

Akikabidhi msaada huo kwa mkuu wa wilaya ya Magu - Karen Kemilembe , Mkurugenzi wa NMB – Ineke Bussemaker  alisema katika mkakati wa benki , inatambua umuhimu wa jamii inayoizunguka na hivyo kutenga kiasi cha bilioni moja na nusu kwaajili ya kusaidia elimu, afya, utoaji elimu ya kifedha na kusaidia wananchi wanapopatwa na majanga mbalimbali kama mafuriko.

 

NMB inajivunia mtandao wa matawi wenye matawi zaidi ya 176 na ATM zaidi ya 600 nchi nzima huku asilimia 70 ya matawi hayo yakiwa maeneo ambayo hakuna benki yenye tawi yaani maeneo ya vijijini.