Wateja zaidi ya 300 kupata huduma kila siku katika Matawi hayo.

Benki ya NMB imefungua matawi mawili ya NMB Katoro na NMB Nyamongo kanda ya ziwa katika mikoa ya Geita na Mara nakufanya jumla ya matawi ya NMB kanda ya ziwa kwa mikoa ya Mara, Mwanza, Geita na Kagera kufikia matawi ishirini na nne.

 

 

 

 

Afisa Tawala wa wilaya ya Tarime - John Marwa (wa pili kulia) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Tawi la NMB Nyamongo wilayani Tarime mkoani Mara. Tawi hili linafanya NMB kufikisha jumla ya Matawi 176 nchi nzima na ATM zaidi ya 600 na kuifanya benki hiyo kuwafikia watanzania wengi zaidi na wa hali zote mijini na vijijini.  Kulia ni meneja wa NMB kanda ya Ziwa - Abraham Augustino na kushoto ni Meneja Mwandamizi wa  Mitandao ya Matawi ya NMB - Gabriel Ole-Loibanguti na Paul Kangele Meneja wa tawi la NMB Nyamongo.

 

 

NMB imekua ikiongeza matawi mengi katika azma yake ya kuwafikia watanzania wote na kuendelea kuwa benki yenye matawi mengi zaidi nchini ambayo mpaka sasa imefikisha matawi 176 na ATM zaidi ya 600 nchi nzima huku ikijivunia uwepo katika kila wilaya nchini.

 

Matawi hayo mapya ya NMB Nyamongo na NMB Katoro kwa pamoja yanahudumia watanzania zaidi ya 600 kila siku huku ikiwapunguzia adha wananchi wa maeneo hayo ambao wamekuwa wakitembea umbali mrefu kufuata huduma za kibenki. Wakazi wa Nyamongo walikuwa wanasafiri mpaka Tarime kupata huduma za kibenki huku wale wa Katoro mpaka waende Geita ambapo ndiko kulikokuwa na matawi ya benki.

 

 

 

 

Mkuu wa Wilaya ya Geita – Manzie Mangachie (kushoto) akimpongeza Meneja Mwandamizi wa  Mitandao ya Matawi ya NMB - Gabriel Ole-Loibanguti kwenye hafla ya kufungua rasmi tawi la NMB Katoro. Tawi hili linafanya NMB kufikisha jumla ya Matawi 176 nchi nzima na ATM zaidi ya 600 na kuifanya benki hiyo kuwafikia watanzania wengi zaidi na wa hali zote mijini na vijijini. Anayeshuhudia ni Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa - Abraham Augustino.