Benki ya NMB imekabidhi msaada kwa wahanga waMafuriko kwa mkoa wa Iringa – Mafuriko ya Pawagana wahanga wa mafuriko ya wilayani Ruangwa kwakukabidhi vyakula na vifaa mbalimbali vya ujenzivyenye thamani ya shilingi milioni 35.

Msaada huo unakuja wakati maelfu ya familia yakiwahayana makazi na chakula baada ya kukumbwa namafuriko yaliyoharibu  mindombinu, nyumba, vyakula pamoja na mashamba yao.

 

 Meneja wa kanda ya kusini NMB , Lilian Mwinula akimkabidhi mkuu wa wilaya ya Ruangwa Mheshimiwa Mariam Mtina  sehemu ya msaada uliotolewa na Benki ya NMB kwa ajili ya wahanga wa mafuriko yalioikumba wilaya ya Ruangwa hivi karibuni .

Katika kuhakikisha kuwa NMB inaendelea kuwakaribu zaidi na watanzania ambao ndio wateja wake wakubwa, miongoni mwa vitu vilivyokabidhiwa kwawahanga ni pamoja na unga, maharage, Mabati, Magodoro, mafuta vyote vikiwa na thamani ya shilingiMilioni 35.

Akikabidhi msaada huo, Mkuu wa kitengo cha biasharaza serikali wa NMB – Bi Domina Feruzi alisema kuwaNMB kama ilivyokawaida yake imeguswa na athari zilizoachwa na mafuriko mkoani Iringa katika kata yaPawaga na hivyo kuitikia mwito wa kusaidia wahangawa mafuriko hayo.

“leo tunakabidhi msaada kwa wahanga hapa Pawagawenye thamani ya shilingi milioni 20 – kwa kutoamagodoro, mabati na vyakula kama unga na maharageambayo tunaamini yatawasongeza siku hizi kabla yakutengemaa kwenye shughuli zao za kila siku,” alisema Bi Domina.

 Meneja wa kanda ya kusini NMB , Lilian Mwinula akimkabidhi mkuu wa wilaya ya Ruangwa Mheshimiwa Mariam Mtina  sehemu ya msaada uliotolewa na Benki ya NMB kwa ajili ya wahanga wa mafuriko yalioikumba wilaya ya Ruangwa hivi karibuni .Msaada huo wenye thamani ya shilingi milioni kumi ulikabidhiwa hivi karibuni  kwa wahanga wa mafuriko hayo.Wengine katika picha ni wakazi wa Ruangwa wakishuhudia makabidhiano hayo.

Kwa upande wake, Meneja wa NMB Kanda ya Kusini– Bi Lilian Mwinula alisema kuwa wameamuakusaidia wahanga wa mafuriko ya wilayani Ruangwaili kupunguza maumivu ya wakazi wa Ruangwayanayotokana na kupoteza mali mbalimbali ambazo sirahisi kuzirudisha mapema.

“tunawapa pole sana wakazi wa hapa Ruangwa kwamajanga yaliyowapata, tumeona tuje hapa kusaidianakwa hali na mali kwani nyinyi ni sehemu yetu na sisi  nisehemu yenu, hivyo kutukimbilia sisi wakati mkiwa nashida ni muhimu sana, Tumeonyesha ubinadamu wetukwa kutoa vifaa hivi yaani mabati, magodoro, mahindi na unga vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni10,” alisema bi Lilian.

Wakati huo huo, NMB imetoa Mahema kwaajili yakusaidia wagonjwa kwenye mlipuko wa ugonjwa wakipindu Pindu mkoani morogoro lenye thamani yuashilingi milioni 5. 

NMB ni benki pekee nchini yenye mtandao mpana wamatawi nchi nzima na ipo katika kila wilaya yenyejumla ya matawi 176 na ATM 600.