Benki ya NMB imekabidhi msaada wa Madawati 70, Vitanda 44 na Magodoro 78 kwa shule ya sekondari Namwai iliyopo Wilayani Siha- Kilimanjaro.Msaada huo una thamani ya shilingi milioni 20 na umekuja kutokana na mahitaji ya shule kwa wakati huu.

 

 

Msaada huo ni moja ya ushiriki wa benki ya NMB katika kuchangia maendeleo hususani kwenye sekta ya Elimu.Benki ya NMB inatambua kuwa ni kupitia jamii ndipo wateja wao wengi wanapotoka, kwa hiyo kurudisha sehemu ya faida kwa jamii ni utamaduni wa kawaida kwao. Kwa mwaka 2016, NMB imetenga zaidi ya shilingi bilioni 1 kwaajili ya kuchangia maendeleo ya wananchi ikiwemo kusaidia sekta ya afya na elimu. Kiasi hiki kinaifanya NMB kuwa benki ya kwanza katika kuchangia maendeleo kuliko benki yoyote nchini.

 

 

 

 

Mkuu wa wilaya ya Siha - Dk Charles Mlingwa(kushoto)akipeana mkono na Meneja wa tawi la benki la NMB Siha -Jovin Twesige(kulia)baada ya Meneja wa NMB,Kanda ya Kaskazini, -Salie Mlay kukabidhi misaada hiyo juzi kwenye shule ya Sekondari Namwai.Picha na Mpiga picha wetu