- Zoezi hili litaendeshwa na NMB kwenye kurasa zao za Facebook, Instagram, Twitter na kwenye tovuti. Shule/ hospitali zitakazohitimu zitakabidhiwa vifaa kama vitanda vya wagonjwa, vitanda vya kujingulia au vifaa vya kuezeka kulingana na taratibu zetu za huduma kwa jamii.
Washiriki wanakubaliana na miongozo ifuatayo:
- Kushiriki kwenye shindano hili, mshiriki anatakiwa kuwa na umri wa miaka 18 na kuendelea.
- Mshiriki atatakiwa kuchagua shule/ hospitali iliyo karibu naye yenye uhitaji wa vifaa vya kuezeka au vitanda vya wagonjwa na vya kujifungulia (atatakiwa kuambatisha picha ya uthibitisho wa mahali alipo).
- Shule/ hospitali itakayochaguliwa ni sharti iwe ya umma (ambatanisha mawasiliano ya shule/ hospitali).
- Mshiriki atatakiwa kupakua ‘template’ kutoka kwenye tovuti yetu https://www.nmbbank.co.tz/csr kisha kujaza fomu na kuwasilisha kwenye This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. pamoja na taarifa zao kamili za mawasiliano.
- Maombi yote yatathaminishwa kupitia matawi yetu ya NMB kulingana na mahali yalipotolewa.
- Shule/ hospitali inatakiwa kuwa inafanya kazi kwa muda mrefu na siyo iliyoanzishwa hivi karibuni.
- Mshiriki atatakiwa kutu’like’ na kutufuata kwenye mojawapo ya kurasa zetu za Facebook, Twitter na Instagram.
- NMB inayo haki ya kumbatilisha mshiriki (na kumchagua mshiriki mwingine) kama wanayo sababu kwamba hajakidhi vigezo au amekwenda kinyume na miongozo.
- Baada ya vifaa kuwa tayari, mshiriki atapewa taarifa ya hatua za makabidhiano.
- Endapo kutatokea kutoelewana kuhusu hatua, utendaji, matokeo na masuala yote kuhusu shindano hili, NMB (au wakala wake aliyeidhinishwa) watakuwa na maamuzi ya mwisho.