KLIK BROCHURE

Safari Yetu

Kwa miaka iliyopita hadi sasa, NMB imekuwa katika safari ya matumizi ya teknolojia mpya, katika kuboresha michakato ya shughuli za kibenki, mifumo ya kutatua matatizo, kuongeza ufanisi, kupunguza gharama za uendeshaji na hivyo kuongeza uzalishaji kwa manufaa ya mteja wetu kupata huduma bora kwa gharama nafuu.

Kutoka katika utamaduni wa zamani wa ufunguaji akaunti, hadi kuingia zama za kubenki kidijitali na NMB Mobile; ni safari isiyo na mwisho, inayoendelea kutafuta na kutumia teknolojia mpya kuboresha uzoefu wa matumizi ya mteja wetu.

Tunayo fahari ya kufikia hatua katika hii zama ya mapinduzi ya kidijitali ambapo tumefanikiwa kubadili jadi ya utamaduni wa zamani wa kibenki na kuingia katika mtindo mpya na wa kisasa kabisa wa huduma za kibenki!

Kamata Mchongo wa KLIK!

Sasa unaweza kupata huduma zote za kibenki muda wowote, popote kwa kubofya tu- na matakwa yako yametimia kwani tumekuletea NMB KLIK!

Sasa unaweza kuweka amana, kufanya miamala, kukopa na kufungua akaunti kamili ya benki- Chap Chap kwenye simu yako kwa USSD (*150*66#) au kupitia App yetu mpya- NMB KLIK!

Rahisi… Haraka… na inayokufaa kabisa kwa hali yoyote… ndizo nguzo katika mapinduzi ya kidijitali zinazohitajika na kutamaniwa na wateja wa biashara yoyote; na sasa imekufikia- NMB KLIK!

Jiunge na jamii ya wajanja wa teknolojia, wabunifu, wa kisasa na watu flani poa kabisa wa familia ya NMB wanaoamini na kufurahia huduma bora za kibenki zinazopatikana kwa wepesi, haraka na urahisi kabisa- NMB KLIK!

Furahia KLIK!

Ni muda wa kuingia na kujikita katika mtindo mpya wa maisha wa viwango bora na vya kisasa vya huduma za kibenki; piga *150*66# -au kwa wepesi zaidi- pakua NMB KLIK! App mpya kutoka Apple Store au Google Play; katika simu yako- huduma iko umbali wa kubofya tu!

  • Fungua Akakunti yako Chap Chap

Ukiwa na namba yako ya simu iliyosajiliwa na kitambulisho halali tu, unaweza ku- KLIK! kufungua na kusajili akaunti yako kamili ya (NMB) Benki Chap Chap muda wowote, popote- na kujipatia sehemu rafiki, Karibu na salama ya kuweka amana na akiba yako!

  • Fanya Miamala Chap Chap

Kupata viwango vya fedha za kigeni; kuhamisha fedha kutoka/kwenda katika akaunti yako kutoka/ kwenda akaunti nyingine ya NMB, akaunti za benki nyingine/mitandao ya simu; kufanya malipo ya bili, kodi, ushuru au manunuzi; kununua muda wa maongezi, LUKU & king’amuzi… sasa ni ku- KLIK! kwa Master-Pass au VISA on Mobile na kulipa Chap Chap!

  • Kopa Chap Chap

Ishi bila stress wala Wasiwasi kwa huduma za mikopo zinazopatikana papo kwa hapo kiganjani mwako. KLIK! kupata salary advance yako muda wowote, popote ndani ya masaa 24 tu. Kwa NMB Wakala wetu pia, sasa mnaweza kupata mkopo wa Wakala popote ulipo bila kulazimika kuacha shughuli zako- ni mwendo wa ku- KLIK! tu kiganjani mwako. Na kukurahihisishia zaidi mchakato wa kuomba mkopo- kipo kikokotozi cha mkopo kwa ajili yako!

(Insert graphics of ‘How To’ for App Download, Account Opening, & Fund Transfer)

Karibu Yako

Ni matarajio yetu utatumia kwa ukamilifu kila huduma tunayokuletea katika zama hii mpya ya kubenki kidijitali na NMB. Na japokuwa tunaelewa kutokana na ufanisi wa mapinduzi haya ya kupata huduma zote za kibenki kiganjani mwako, yamkini usiwe na sababu ya kubanduka kwenye simu yako; usipotee sana, tutafurahi na kushukuru ukiweza kututembelea katika tawi letu lililopo karibu nawe ndani ya siku 90 baada ya kupata akaunti yako, tufahamiane zaidi na kupata mrejesho wako kuhusu huduma zetu.

Pia katika kuhakikisha unafurahia huduma zetu bila tatizo lolote, iko tayari muda wote kukuhudumia kwa taarifa zaidi juu ya huduma zetu na vidokezo vya kufurahia huduma za KLIK! kiulaini zaidi- tembelea ukurasa wa Msaada katika orodha ya USSD/App; au www.nmbbank.co.tz/nmbapp au tupigie 0800 002002 bure!

The Rubik's Cube solver calculates the rotations to sove the unsolvable cube.