Kudaka fursa hii kabambe ya kufanya kazi na NMB Bank kama wakala wetu, unatakiwa kuwa na vigezo vifuatavyo:

  • Unatakiwa kuwa na biashara endelevu na imara, au shughuli yoyote halali na yenye leseni hai
  • Unatakiwa kua na Biashara inayoendeshwa kwenye sehemu ya kudumu na rasilimali watu ili kuhakikisha unatoa huduma kwa ufanisi na usalama
  • Biashara inatakiwa kuwa inafanya kazi kwa angalau miezi 18 kama itakavyothibitishwa na leseni zilizopita na/au nyaraka nyingine za usajili, kabla ya tarehe ya maombi ya kuwa wakala
  • Biashara au Mmiliki hatatakiwa kuwa ameorodheshwa kama mdeni asiyelipa kwenye benki yoyote na/au taasisi ya kifedha na atatakiwa kuzingatia hilo katika muda wote wa mkataba ya uwakala
  • Sio ruhusa kuendesha uwakala wa benki kama biashara pekee
  • Wafanyakazi wa NMB Plc na washirika wao hawataruhusiwa kufanya uwakala kwa niaba ya benki
  • Unahitaji kuwa na mtaji wa kazi wa kuanzia Tsh milioni 2 au zaidi ambayo haitapungua kwa muda wote wa uwakala na ada ya uwakala ya Tsh 200,000 isiyorudishwa baada ya wakala kuidhinishwa na kusaini mkataba.

Kama unakidhi vigezo vyote hapo juu, tafadhali tembelea tawi lilio karibu yako na/au jaza fomu iliyopo chini, na ofisi yetu itawasiliana na wewe na kukupatia fursa hii kubwa.